Yesu katika sanaa
Sehemu ya mfululizo kuhusu |
Ukristo |
---|
|
|
Yesu katika sanaa mbalimbali ameshika nafasi kubwa katika uchoraji, uchongaji, muziki n.k. vya milenia mbili tangu azaliwe.
Picha
[hariri | hariri chanzo]Picha za Yesu Kristo zilitokeza mapema kwa namna nyingine jinsi Ukristo ulivyosogea mbali na Uyahudi uliopinga uchoraji wa Mungu na viumbe vyake kwa jumla.
Kwanza Yesu hakuchorwa, ila aliwakilishwa na ishara mbalimbali, kama vile samaki (kwa Kigiriki jina la samaki lilitumika kwa kuchukua kile herufi yake kama mwanzo wa neno zima lililomhusu: Yesu Kristo Mwana wa Mungu Mwokozi), Mchungaji mwema, Mfalme, Mwalimu.
Baadaye alianza kuchorwa kama kijana asiye na ndevu (hadi karne VI, lakini kuanzia karne IV hata akiwa na ndevu na nywele ndefu kama ilivyozoeleka zaidi baadaye.
Kutokana na mabishano ya karne VII na karne VIII kuhusu uhalali wa picha, katika Ukristo wa mashariki namna ya kumchora iliratibiwa.
Kumbe katika Ukristo wa magharibi Karne za Kati zilileta mwelekeo mpya, wa kibinadamu zaidi, hasa kwa kufuata mvuto wa imani kwa Yesu wa historia, yaani jinsi alivyoishi duniani.
Hatimaye katika Renaissance Kristo alianza kuchorwa kama kielelezo cha mtu mkamilifu hata upande wa sura.
Mifano ya michoro
[hariri | hariri chanzo]-
Mchoro wa ukutani katika handaki la Commodilla ukiwa katika ya ile ya kwanza kumuonyesha Yesu ana ndevu, mwisho wa karne ya 4.
-
Kristo Pantokrator ya karne ya 11.
-
Kristo kama Mtu wa Mateso kadiri ya Andrea Mantegna.
-
Touchdown Jesus karibu na Hesburgh Library.
-
Kristo akisulubiwa kadiri ya Titian.
-
Mchoro wa Francesco Trevisani kuhusu ubatizo wa Yesu, 1723.
-
Picha takatifu ya Pantokrator kutoka Russia ya karne ya 19.
-
Picha takatifu ya Kiorthodoksi ya "Kristo Mwenye Huruma".
Mifano ya sanamu
[hariri | hariri chanzo]-
Kristo Mfalme huko Ureno.
-
Cristo de la Concordia huko Bolivia, inayodaiwa kuwa sanamu ya Yesu iliyo kubwa kuliko zote zilizowahi kutengenezwa.
Mifano mingine
[hariri | hariri chanzo]-
Mozaiki ya karne ya 3 ikimuonyesha Yesu kama Jua lisiloshindika katika Mahandaki ya Vatikano chini ya Basilika la Mt. Petro.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Construction progressing on new Jesus statue along I-75", WCPO, 15 June 2012. Retrieved on 7 September 2012. Archived from the original on 2013-06-29.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Pictures of Jesus Perhaps Derived from the Shroud of Turin Archived 4 Machi 2012 at the Wayback Machine. December 2005
- Warner Sallman's Head of Christ: An American Icon
- Is this the real face of Jesus Christ?
- Images of Christ – the Deesis Mosaic of Hagia Sophia
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yesu katika sanaa kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |